Zilipendwa ni neno linalotumika kutaja vitu vilivyopitwa na wakati, lakini vilikuwa na wapenzi wengi sana kiasi kwamba hata ukisikia au kuviona tena leo utakumbuka wakati wako. Istilahi hii imetumika sana katika nyimbo na filamu. Kumekuwa hadi na vipindi vya TV na Redio katika Afrika ya Mashariki vinavyozungumzia Zilipendwa. Karibia katika kila redio nchini Tanzania kuna kipindi maalumu cha Zilipendwa.