Kama unajua kitu, ukisambaze. Kama kuna kitu ambacho hukijui, anzisha utafiti.
— Kutoka toleo la mwaka 1772 la Encyclopédie; Ukweli, juu katikati, ukizungukwa na mwangaza na ukionyeshwa wazi na falsafa na akili (kulia).

Zama za Mwangaza (au Falsafa ya mwangaza au Mwangaza au Wakati wa akili) ni jina la vuguvugu la kiutamaduni hasa katika karne ya 18 barani Ulaya.

Kituo chake kikuu kilikuwa nchini Ufaransa kikiongozwa na wanafalsafa wawili ambao ni Voltaire na Denis Diderot. Huyo alieneza azimio la mwangaza kwa kutumia mfululizo wa Encyclopédie, kitabu kikubwa cha kwanza cha kumbukumbu.

Azimio muhimu zaidi la mwangaza lilikuwa ni kuamini watu kwa sababu. Watu wote wana uwezo wa kujifikiria. Kwa hiyo, mtu hapaswi kuamini vitu kwa nguvu ya kimamlaka. Watu hawatakiwi kuamini kinachofundishwa na Kanisa wala kile anachofundisha mchungaji.

Azimio lingine muhimu ni kwamba jamii imeendelea vyema kwamba wanachama wake wote wana vyeo sawa tu, hamna ubaguzi, wanashirikiana sawa tu katika usanifu.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Tapo hilo la falsafa lilianza mwishoni mwa karne ya 17 na kuenea katika karne ya 18 katika Ulaya nzima na hatimaye Marekani likisisitiza akili na nafsi ya mtu kuliko mapokeo.[1]

Lengo lilikuwa kurekebisha jamii kwa kufuata uelewa wa akili, hasa kupitia mbinu za sayansi, si desturi na mafundisho ya imani, hasa ya Kanisa Katoliki.

Ilifanya wengi wapate wasiwasi kuhusu dini na wazingatie zaidi sayansi,[2] ikiathiri historia yote iliyofuata hata upande wa siasa.

Kati ya watu walioisambaza, muhimu zaidi ni wanafalsafa Baruch Spinoza (16321677), John Locke (16321704), Pierre Bayle (16471706), Voltaire (16941778) na nwanafizikia Isaac Newton (16431727).[3]

Mara nyingi watawala waliunga mkono watu kama hao wakajaribu kutekeleza maelekezo yao kwa serikali.

Baada ya mwaka 1800 watu wengi walianza kushtukia matokeo yake (hasa Mapinduzi ya Kifaransa) na kuelekea upande mwingine, ule wa hisia.[4]

Tanbihi

[hariri | hariri chanzo]
  1. "enlightenment". Oxford Dictionaries. Oxford University Press, n.d. Web. 19 September 2013.
  2. Kors, Alan Charles. Encyclopedia of the Enlightenment. Oxford: Oxford UP, 2003. Print.
  3. Sootin, Harry. "Isaac Newton." New York, Messner(1955).
  4. Casey, Christopher (Oktoba 30, 2008). ""Grecian Grandeurs and the Rude Wasting of Old Time": Britain, the Elgin Marbles, and Post-Revolutionary Hellenism". Foundations. Volume III, Number 1. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-05-13. Iliwekwa mnamo 2009-06-25.((cite web)): CS1 maint: date auto-translated (link)

Marejeo

[hariri | hariri chanzo]

Ya jumla

[hariri | hariri chanzo]

Ya dhati zaidi

[hariri | hariri chanzo]

Vyanzo vikuu

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zama za Mwangaza kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.