Wongofu wa Mtume Paulo akielekea Damasko (mchoro ≥wa Caravaggio).
Agano Jipya

Waraka wa pili kwa Wathesalonike ni kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.

Ni barua ya Paulo wa Tarso kwa ushirika wa Wakristo katika mji wa Thesalonike (Ugiriki wa Kale).

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mazingira

Miezi michache baada ya Mtume Paulo kuwaandikia Wakristo wachanga wa Thesalonike barua tulivu, akarudia kuwaandikia kutokana na taarifa nyingine zilizomtia tena wasiwasi.

Akawafafanulia zaidi Ujio wa pili wa Bwana na dalili zake, akiwahimiza hasa kufanya kazi kwa bidii na kuwajibika wakati wa kungojea ujio huo wa Yesu badala ya kuiacha kwa kisingizio cha kwamba, eti Kristo amesharudi (2Thes 2:1-15; 3:6-15).

Mpangilio

Mpangilio wa barua hizo ni uleule wa barua zitakazofuata: baada ya salamu na shukrani kwa Mungu, yanafuata mafundisho ya imani, halafu maadili, na hatimaye salamu nyingine.

Marejeo

Viungo vya nje

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Waraka wa pili kwa Wathesaloniki
Search Wikisource Wikisource has original text related to this article:

Tafsiri ya Kiswahili

Vingine

Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waraka wa pili kwa Wathesaloniki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.