Waraka wa karatasi.

Waraka (kwa Kiingereza: document) ni hati yenye taarifa maalumu. Kwa kawaida, siku hizi waraka unaandikwa katika karatasi.

Katika Biblia ya Kikristo mna nyaraka mbalimbali ambazo pamoja na barua zinafikia idadi ya 21, kwa mfano: Waraka kwa Waebrania.

Katika utarakilishi, waraka pepe (kwa Kiingereza: electronic document) ni hati pepe inayotumika katika tarakalishi. Waraka pepe ni kama waraka wa kawaida ila data ni za elektroniki.

Marejeo