Wakazakhi (kwa Kikazakhi Қазақ/Qazaq, wingi Қазақтар/Qazaqtar) ni taifa lenye kutumia Kikazakhi, mojawapo ya lugha za Kiturki linalopatikana hasa nchini Kazakhstan, lakini pia katika Mongolia, China, Urusi, Uzbekistan na Afghanistan. Vikundi vidogo zaidi vinapatikana Iran na Uturuki.
Idadi ya Wakazakhi hukadiriwa kuwa mnamo milioni 20.
Upande wa dini walio wengi ni Waislamu Wasunni.
Wakazakhi wametokea katika historia ya makabila ya Kiturki katika Asia ya Kati. Jina "Kazakh" linamaanisha "huru, asiyetawaliwa": lilikuwa namna ya kutaja makabila ya Waturki waliopendelea kufuata mila zao na kujitenga mnamo 1450 na milki ya Wauzbeki.
Maeneo makubwa walipoishi Wakazakhi yalitwaliwa na Urusi kuanzia karne ya 17 kwa hiyo Wakazakhi wengi waliishi katika Milki ya Urusi na katika karne ya 20 katika Umoja wa Kisovyeti.
Baada ya mapinduzi ya kikomunisti Wakazakhi walipewa eneo lao la pekee ndani ya mfumo wa ukomunisti na tangu mwaka 1936 eneo hili lilikuwa Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kikazakhi, moja kati ya jamhuri 17 zilizounda Umoja wa Kisovyeti. Hiyo ilipata uhuru wake tangu kuporomoka kwa ukomunisti mwaka 1991.
Leo hii wanaishi