Utendi (pia: utenzi; kutoka kitenzi "kutenda") ni aina ya ushairi na tanzu mojawapo ya fasihi simulizi. Kwa kawaida, utendi husimulia maisha na matendo ya mhusika shujaa au wa visasili[1].

Maarufu katika fasihi ya Ulaya, kuna tendi kama wimbo wa Troya, wimbo wa Odisei na wimbo wa kabila la Nibelungi; India kuna wimbo wa Mahabharata; Afrika kuna utendi wa Sundiata na wimbo wa Oduduwa. Hizo zote mara nyingi hudondolewa kama mifano ya utendi.

Siku hizi hata riwaya au filamu, hasa kama ni ndefu sana pamoja na wahusika wengi au nyakati nyingi, huitwa utendi.

Kwa Wakristo wanaotumia Kiswahili tahajia "utenzi" inataja hasa nyimbo za kiroho.

Tenzi maarufu za Kiswahili

Tanbihi

  1. Knappert (1967)

Marejeo

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Utendi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.