Ushindi (kutoka kitenzi kushinda, yaani kubaki; kwa Kiingereza: victory) ni neno linalomaanisha kufanikiwa au kufaulu katika matukio kama vile majaribu, mitihani, kesi, mapigano au mechi.
Katika Ukristo ushindi mkuu ni ule alioupata Yesu kwa ajili ya watu wote dhidi ya mauti kwa kufufuka kwake.[1]