Ukambi | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Specialty | Infectious diseases |
ICD-10 | B05. |
ICD-9 | 055 |
DiseasesDB | 7890 |
MedlinePlus | 001569 |
eMedicine | derm/259 emerg/389 ped/1388 |
MeSH | D008457 |
Ukambi (au surua) ni ugonjwa wa kuambukiza unaoenezwa sana kupitia mgusano yanayosababishwa na virusi vya ukambi.[1][2]
Ishara na dalili za kwanza kwa kawaida hujumuisha homa, ambayo mara nyingi huwa zaidi ya °C 40 (°F 104.0), kikohozi, mafua, na macho mekundu.[1][3] Siku mbili au tatu baada ya dalili kuanza, madoa madogo meupe yanaweza kuonekana ndani ya kinywa yanayojulikana kama alama za koplik. Chunusi nyekundu, zinazoanza kwenye uso kisha kuenea kwa mwili wote, kwa kawaida huanza siku tatu hadi tano baada ya mwanzo wa dalili.[3]
Dalili kwa kawaida huwa siku 10–12 baada ya kutangamana na mtu aliyeambukizwa kwa siku 7–10.[4][5]
Matatizo zaidi ya ukambi hutokea kwa takriban asilimia 30 na yanaweza kujumuisha kuhara, upofu, inflamesheni ya ubongo, na nimonia miongoni mwa mengine.[4][6]
Rubela na roseola ni magonjwa tofauti ingawa yanafanana na surua.[7]
Ukambi ni ugonjwa unaoambukiza kupitia hewa na kuenezwa kwa urahisi na watu walioambukizwa kupitia kikohozi na kupiga chafya. Pia unaweza kuenezwa kupitia kutangamana na mate au makamasi.[4] Watu tisa kati ya kumi wasio na kingamwili wanaokaa pamoja na mtu aliyeambukizwa wataambukizwa ukambi. Watu huweza kuwaambukiza wengine katika siku nne kabla hadi siku nne baada ya mwanzo wa chunusi.[6]
Watu kwa kawaida hupata ugonjwa huu mara moja tu.[4] Vipimo vya virusi hivi katika visa vinavyokisiwa ni muhimu kama sehemu ya juhudi za afya ya umma.[6]
Chanjo ya ukambi huwa mwafaka katika kuzuia ugonjwa huu. Uchanjaji umepunguza asilimia 75 ya vifo vilivyotokana na ukambi kati ya miaka ya 2000 na 2013 na takriban asilimia 85 ya watoto ulimwenguni kote wanapata chanjo kwa sasa.
Hakuna matibabu maalum ya ukambi. Hata hivyo, utunzaji wa kimsaada unaweza kuboresha matokeo.[4] Hii inaweza kujumuisha kuwapa wagonjwa mmumunyo wa chumvi-maji za kunywa (viowevu vyenye utamu na chumvi), vyakula vyenye afya na dawa ya kupunguza homa.[4][5] Antibiotiki zinaweza kutumika ikiwa maambukizi ya bakteria kama vile ya numonia yatatokea. Nyongeza ya Vitamini A hupendekezwa katika nchi zinazoendelea.[4]
Ukambi huathiri takriban watu milioni 20 kila mwaka,[1] hasa katika maeneo yanayoendelea barani Afrika na Asia.[4] Ukambi husababisha vifo vingi vinavyoweza kuzuiwa kwa kutumia chanjo ikilinganishwa na magonjwa mengine.[8] Ukambi ulisababisha takriban vifo 96,000 katika mwaka wa 2013 ikilinganishwa na vifo 545,000 katika mwaka wa 1990.[9] Katika mwaka wa 1980, ugonjwa huu ulikadiriwa kusababisha vifo milioni 2.6 kila mwaka.[4] Kabla ya uchanjaji nchini Marekani, kati ya visa milioni tatu na milioni nne vilitokea kila mwaka.[6] Watu wengi wanaoambukizwa na kufariki huwa wenye umri wa chini ya miaka mitano.[4] Hatari ya kifo kwa walioambukizwa kwa kawaida huwa asilimia 0.2,[6] lakini hii inaweza kuongezeka hadi asilimia 10 kwa wale walio na utapiamlo.[4] Ukambi hauaminiki kuathiri wanyama.[4]
((cite web))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
((cite web))
: External link in |website=
(help)CS1 maint: date auto-translated (link)
((cite web))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
((cite web))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
((cite book))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
((cite book))
: |edition=
has extra text (help)
((cite journal))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
((cite journal))
: |first1=
has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link)