Uchale (pia undugu wa uchale au undugu wa kuchanjiana) ni undugu unaofanywa kati ya watu wawili ambao hawana undugu wa kuzaliwa kwa kuchanjiana damu.
Mviga wa uchale na sababu zake hutofautiana kulingana na mila na tamaduni za watu wanaofanya undugu namna hiyo[1][2].
Leo, uchale hufanyika katika magenge[3] na baadhi ya vikundi vya uhamasishaji[2].
Katika jamii za Waafrika ambako uchale ulifanyika, ulitumika kama mkataba[5][6][7] au njia ya kuanzisha uhusiano[8] kati ya wanaume wawili au jamii[6]. Undugu wa aina hii haungevunjika ovyo. Kutoheshimu ndugu wa uchale, kuliaminika kuwa na adhabu ya kiungu[1].
Sababu za kufanya undugu huo zilihusiana wanaume kutaka kulinda mali na kutaka kuhakikisha heshima baina ya ndugu. Kwa mfano, katika jamii za watu wa Kigezi, Uganda, wanaume waliingia katika uchale ili waweze kupitia njia za biashara kwa usalama[7]. Machifu wa jamii za Watio na Wabhobangi walichanjiana ili washirikiane katika raslimali za Mto Kongo[6]. Katika jamii ya Wakikuyu, watu ambao hawakuwa Wakikuyu hawakukubalika hadi wakati mviga wa uchale ufanyike[9][8].
|date=
(help)
|date=
(help)
|pmc=
value (help). PMID 25610258. doi:10.5152/eajm.2013.16. Check date values in: |date=
(help)
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uchale kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |