Makao Makuu | Buguruni, Dar es Salaam, Tanzania |
---|---|
Mapato | bilioni TSh 176 (March 2013) |
Total equity | bilioni TSh487 (March 2013)[1] |
Mmiliki | AB InBev |
Tanzania Breweries Ltd ni kampuni nchini Tanzania inayohusika katika uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa bia, pombe mbalimbali na vinywaji visivyo na kilevi nchini Tanzania.
Makao makuu ya TBL yapo . Kampuni inaendesha viwanda vinne Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya. [2]
TBL imeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam. Mmiliki wa kampuni ni SABMiller wa Afrika Kusini.
Kampuni hiyo ilianzishwa mnamo 1933 kwa jina la Tanganyika Breweries wakati wa ukoloni wa Kiingereza. Ikanunuliwa kampuni ya Kenya Breweries Limited (KBL, Nairobi) mnamo 1935. Tangu 1936, makampuni yote mawili yaliunganishwa kuwa East African Breweries Limited (EABL).
Mnamo mwaka wa 1964, jina la kampuni upande wa Tanzania lilibadilishwa kutoka kuwa Tanzania Breweries Limited kufuatia maungano wa kisiasa wa Tanganyika na Zanzibar.
Mwaka 1967 Serikali ya Tanzania ilianza kuekeza hapa ikanunua asilimia 45 za hisa. Baadaye serikali iliendelea kutaifisha kampuni yote na kuiendesha kama kampuni ya umma kulingana na msimamo wa Azimio la Arusha . [3] Baada ya kutaifishwa mnamo 1967, TBL ilisimamiwa vibaya ikaendelea kuleta hasara kibiashara; ubora wa bia zake ulishuka pia ilishindwa kutengeneza bidhaa za kutosheleza soko la nchi.
Mnamo 1993 serikali ya Tanzania iliingia katika ubia na ushirikiano na <a href="https://en.wikipedia.org/wiki/South_African_Breweries" rel="mw:ExtLink" title="South African Breweries" class="cx-link" data-linkid="102">South African Breweries International</a> (sasa SABMiller) iliyokabidhiwa utawala wa TBL. SABl waliwekeza dolar za Kimarekani milioni 22.5 katika TBL na kupata hivyo kumiliki asiimia 50 za TBL. Utawala wa SABMiller ulifaulu kuondoa hitilafu ya awali na kuongeza uzalishaji wa bia mara tatu katika kipindi cha miaka mitatu iliyofuata. [4]
Kwenye Septemba 1998 TBL iliorodheshwa tena kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Mnamo 2002, EABL ya Kenya ilinunua asilimia 20 za hisa za TBL, na kusaini mikataba ya leseni na kampuni ya SABl ya Afrika Kusini. Pande mbili zilipatana kugawa soko la Afrika ya Mashariki kati yao; EABL ilikabidhi kiwanda cha bia cha Kibo kwa TBL, na SABl iliondoka katika soko la Kenya [5]. Kufuatana na mapatano haya TBL ilishika asilimia 98% za soko la bia nchini Tanzania ifikapo mwaka 2004. [6]
Mnamo mwaka wa 2010, EABL iliiliondoka katika makubaliano haya na TBL, ikauza hisa zake na kununua hisa za asilimia 51 katika Serengeti Breweries, ambayo ni mtengenezaji wa bia mkubwa wa pili nchini Tanzania. [7]
Mnamo Machi 2013, TBL ilinunua asilimia 60 za hisa za Darbrew Limited kwa TShs 8,816 Milioni na kupata udhibiti wa kampuni hiyo inayopika pombe za kienyeji. [6]
Mnamo Machi 31, 2013, TBL ilishika asilimia 74 za soko la vinywaji vya pombe nchini Tanzania. Iliuza viwango vikubwa vya bia nje kwa Nile Breweries Limited ya Uganda, Crown Beverage Limited ya Kenya na Zambia Breweries Limited ya Zambia, ambazo zote zinamilikiwa na SABMiller . [6]
Mwaka 2016 SABMiller ilinunuliwa na kampuni la Marekani AB InBev (Anheuser-Busch InBev SA/NV)[8].
Kampuni yaliyo chini ya Tanzania Breweries Limited ni pamoja na: [6]
Kwa sasa TBL inauza aina 11 za vinywaji zikiwa pamoja na:
Hisa za Tanzania Breweries Limited zinauzwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam, chini ya kifupi: TBL .
Kufuatana na taarifa ya mwaka 2018 jumla ya hisa 295,056,063 za kampuni zilimilikiwa na wafuatao [9]:
Wanahisa wa Tanzania Breweries Limited | ||||||||||||||||||||||||||||||
|
Tanzania Breweries Limited inasimamiwa na Bodi ya Wakurugenzi ya watu kumi na Cleopa Msuya anayehudumu kama Mwenyekiti wa kikundi hicho na Philip Redman kama Mkurugenzi Mkuu. [10]
<ref>
tag; no text was provided for refs named History of EABL
|=
ignored (help)