Sharatani (Beta Arietis, Sheratan)
Sharatani (Sheratan) katika kundinyota yake ya Hamali (Aries)
Kundinyota Hamali (Kondoo) (Aries)
Mwangaza unaonekana 2-655[1]
Kundi la spektra A5 V
Paralaksi (mas) 54.74
Umbali (miakanuru) 59.6
Mwangaza halisi 1.55
Masi M☉ A : 2.34 B : 1.34
Mng’aro L☉ A : 23 B : 1.3
Jotoridi usoni wa nyota (K) A : 9000
Majina mbadala <small Al Sharatain, 6 Arietis, Gl 80, HR 553, BD +20°306, HD 11636, SAO 75012, FK5 66, HIP 8903


Sharatani (lat. & ing. Sheratan, pia β Beta Arietis, kifupi Beta Ari, β Ari) ni nyota angavu ya pili kwenye kundinyota ya Hamali (Kondoo) (Aries).

Jina

Nyota ya Sharatani ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [2]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaoijua kama الشرطان ash-sharatan kwa maana ya “alama mbili”; jina hili lilitaja nyota za Beta na Gamma Arietis maana miaka 2000 iliyopita hizi mbili zilionyesha kuja kwa sikusare ya machipuo na hivyo chanzo cha mwaka mpya. [3].

Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota hii kwa tahajia ya "Sheratan" [4].

Beta Arietis ni jina la Bayer ikiwa ni nyota angavu ya pili katika Hamali na Beta ni herufi ya pili katika Alfabeti ya Kigiriki.

Tabia

Sharatani ni nyota iliyopo katika kundi la spectra A inayoyeyunganisha hidrojeni kuwa heliamu. Iko kwa umbali wa miakanuru 60 hivi kutoka kwetu. Ikiwa na jotoridi ya nyuzi za Kelvin 9000 usoni wake ni ni moto kushinda Juan a pia mng’aro wake unazidi ule wa Jua mara 23. Utafiti wa spektra unaonyesha ya kwamba kuna nyota msindikizaji ambao hauonekani kwa darubini ua kuangalia nuru ya kawaida lakini imewezekana kuipima na kuthibitisha hapa kuna nyota maradufu yenye sehemu mbili za A na B.

Tanbihi

  1. Vipimo kufuatana na Pan, X. P.; et al. (1990)
  2. ling. Knappert 1993
  3. Allen, Star-Names (1899), uk. 81
  4. Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017

Viungo vya Nje


Marejeo