Makala haina vyanzo vya kutosha Makala (au sehemu ifuatayo ya makala) inatoa habari bila kuonyesha vyanzo au uthibitisho wowote. Ona namna ya kutaja vyanzo hapa: Wikipedia:Umaarufu na Kutaja vyanzo. Ni lazima kuboresha makala kwa kutafuta vyanzo na kuvitaja kama marejeo, la sivyo sehemu ya makala au yote kabisa inaweza ikafutwa. Unaweza kuondoa kigezo hiki mara baada ya vyanzo sahihi kuwa vimeingizwa katika makala
Masanduku kwenye jengo la posta

Sanduku la posta (kifupi: S.L.P.; kwa Kiingereza Post Office Box, kifupi: P.O.B.) ni sanduku linalofungwa kwa kitasa linalopatikana katika jengo la posta.

Linakodiwa na mteja anayepokea ufunguo wa sanduku. Kila sanduku huwa na namba yake na namba hiyo ni anwani yake akituma au kupokea barua au vifurushi.

Wakati barua inafika kwenye ofisi husika, inawekwa katika sanduku la posta linalotajwa kwenye bahasha ya barua. Kwa kawaida masanduku hupatikana kwenye sehemu ya jengo la posta inayoweza kufikiwa wakati wote, hivyo mteja anaweza kuchukua barua saa yoyote bila kubanwa na ratiba ya ofisi.

Anwani ya mtaani na anwani ya sanduku la posta

Katika nchi nyingi mteja anaweza kuchagua kama apokee barua nyumbani kwake (akitumia anwani ya mtaa na namba ya nyumba) au kwenye sanduku la posta, au kwa njia zote mbili.

Katika nchi nyingi za Afrika, zikiwa pamoja na Kenya na Tanzania, hakuna huduma ya kupeleka barua za kawaida hadi nyumbani, hivyo sanduku la posta ni njia pekee ya kawaida kupokea barua[1]. Katika nchi hizo ni kawaida kwa watu wengi kutaja namba ya sanduku ya marafiki, shule au ofisi fulani wakihitaji kupokea barua au kifurushi.

Sanduku la posta na msimbo wa posta

Anwani inayoonyesha sanduku la posta na chini yake mahali na msimbo wa posta

Namba ya sanduku la posta lisichanganywe na namba ya msimbo wa posta (au postikodi, kutoka Kiingereza: postal code).

Marejeo

  1. Universal Postal Union. "Kenya" (PDF). Universal Postal Union. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2020-06-13. Iliwekwa mnamo 2016-02-19.

Viungo vya Nje