Peru |
---|
Peru (pia Peruu) ni nchi ya Amerika Kusini upande wa magharibi ya bara.
Imepakana na Ekuador, Kolombia, Brazil, Bolivia na Chile. Kuna mwambao wa Pasifiki.
Peru ilikuwa koloni la Hispania kati ya miaka 1532 na 1821.
Kabla ya kuja kwa Wahispania, Peru ilikuwa kitovu cha Dola la Inka.
Hadi leo kuna idadi kubwa ya Waindio (45%) wanaotunza utamaduni wao, mbali ya machotara Waindio-Wazungu (37%). Utafiti wa DNA yao unaonyesha urithi wa Kiindio umechangia 79.1% za DNA ya wakazi wa leo. Wazungu wenyewe ni 15% tu.
Lugha rasmi ni Kihispania (84.1%), Kiquechua (13%) na Kiaymara (1.7%).
Upande wa dini, Wakatoliki ni 81.3% na Waprotestanti 12.5%.
Nchi na maeneo ya Amerika Kusini |
Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyani ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Peru kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |