Mtawala Njinga.
Eneo la Ufalme wa Ndongo.

Njinga (anaitwa pia: Rainha Ginga, Njinga Mbande, Njinga Mbandi, Jinga, Singa, Zhinga, Ginga, Njingha, Ana Njinga, Ngola Njinga, Zinga, Zingua, Mbande Ana Njinga, Ana Njinga, Njinga wa Ndongo na Matamba; 1583 - 1663) alikuwa mtawala wa Dola la Ndongo na Matamba katika Afrika ya Kati (Angola ya leo). Aliongoza dola hilo miaka 37.

Alikuwa mwanamke mkuu wa bara la Afrika katika karne ya 17.

Maisha yake

Alipambana na Ureno kwa msaada wa Uholanzi miaka 30 na hatimaye akatia saini mkataba nao.

Alibatizwa mwaka 1622, lakini baada ya kumrithi kaka yake (1627) aliasi kabisa na kuongoza muda mrefu. Aliongokea tena Kanisa Katoliki mwaka 1656, jambo lililoshangaza sana waliofahamu maisha yake ya awali. Hapo alijitahidi kugeuza ufalme wake kuwa wa Kikristo, akiagiza watu wahubiriwe na akisimamisha misalaba kila mahali.

Marejeo

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Njinga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.