Kipala, salam. Ndugu naomba niswamehe kwa kuhamisha maelezo yako ya awali katika Kumbukumbu ya Archive-2 bila ya idhini yako. Nilikuwa naona shida wakati wa kuanzisha ujumbe mpya katika kurasa yako ya majadiliano, hivyo nikaone bora niipunguze kwa njia ya kuijaladia!! Natumai utakuwa umeniswamhe kwa hili, kazi njema...--Mwanaharakati (talk) 15:45, 12 Februari 2008 (UTC)
Kipala, salam. Template:Muigizaji, imepatwa na matatizo kidogo. Sijui ni kwanini imekuwa vile ilivyo sasa, lakini hamna mtu aliyetia mkono wake zaidi ya siye wenyewe toka hapo awali. Labda unaweza kuitazama na kuitafutia ufumbuzi. Naomba ichunguze kisha ikinge kabisa...--Mwanaharakati (talk) 16:43, 13 Februari 2008 (UTC)
Basi. Naona kuna msiba wa template zote kwa ujumla. Huenda kukawa na tatizo huko makao makuu ya mradi mzima, maana kila template ninayoigusa naona inakasoro (sielewi na naona kuna ugonjwa wa kifafa kwa template). Tuvute subra labda kuna tatizo kwao!!--Mwanaharakati (talk) 16:51, 13 Februari 2008 (UTC)
KICHEKO. Si mwigizaji wala ya nchi-mto, uainishaji nk. Zote zikomatatani. Kifupi ni msiba wa kitaifa, maana hakuna kilichokaa sawa. Ndugu, hii si ni hatari isiyo na kifani? Iweje template zote ziwe lemavu pasisipo na sababu? Nakumbuka nilimpelekea Marcos baadhi ya pendekezo ya kubadilisha lugha katika sw:wiki, natumai kazi hiyo atakua kesha ianza na ndiomaana lile neno lililo andikwa "Viungo viungacho ukurasa huu" naona hamna. Labda nimwendee tena na kumweleza juu ya tatizo hili au unaonaje?--Mwanaharakati (talk) 07:27, 14 Februari 2008 (UTC)
Bado nabisha. Angalia Ujerumani kisha Aseniki, utaona kama kuna tatizo. Labda kwako hizi nazo zitaonyesha kasoro, endapo hizo kwako zita kaa sawa basi ujue kwangu kweli kua kasoro... nategemea jibu lako..--Mwanaharakati (talk) 11:26, 14 Februari 2008 (UTC)
Naomba angalia hii: Ukiitzama kwa mbali yaonysha template imekaa kulia na haina mzunguko wa kuizungushia (yaani border iko sufuri. Naomba nisaidie..
Naona kwangu kama ni balaa kubwa!!--Mwanaharakati (talk) 13:17, 14 Februari 2008 (UTC)
Salam. Naona faraja baada ya kuona na wewe umeharibikiwa (tehe tehe tehe-kicheko). Sikuwa najisikia vizuri pale nionapo kasoro zile katika Kompyuta yangu tu, na ndiomaana nilikuwa nalia kwa-kuwa ulikuwa unaniambie mashine yangu kimeo. Naona sasa tatizo lisha fika hadi huko Ujerumani uliko. Subra yahitjika. Lakini mie kuunda makala bila ya template (najihisi kama bado mtoto?? Au??) Hapendezi kwa makala ninazo changia!! Ila pole na wewe kwa ugonjwa wa kifafa cha template!! Kazi njema...--Mwanaharakati (talk) 14:18, 15 Februari 2008 (UTC)
Salam. Naomba nisaidie kutafsri neno hili (wagonload) kwa Kiswahili kilicho kizuri na kitasaidia kuleta maana nzuri. Wagonload, najua kama ni wale Farasi walio na kijumba nyuma (ama sivyo?) Kwa Kiswahili kilicho sahihi sipati maana nzuri, kwa hiyo naomba nisaidie kuswahilisha neno hili... Nategemea majibu yako.--Mwanaharakati (talk) 04:54, 16 Februari 2008 (UTC)
Haya basi sentensi yenyewe hii hapa: Set in Mexico under the rule of Emperor Maximilian I, Sabata is hired by the guerilla leader Señor Ocaño to steal a wagonload of gold from the Austrian army. Kazi kwako mkubwa...--Mwanaharakati (talk) 11:12, 16 Februari 2008 (UTC)
Aksante. Jana ilikuwa Ijumaa, lakini huku badilisha ukurasa wa usoni, vipi hukupata muda au?..--Mwanaharakati (talk) 13:07, 16 Februari 2008 (UTC)
Salam. Nimevumilia nimeshindwa. Sasa nakupa pongezi kwa kuwa Mswahili huria aliye na kiwango cha mzawa wa lugha ya Kiswahili, au unaonaje? Nimebadilisha Language Status: Kutoka daraja la tatu hadi (fasaha). Kiwango ulicho nacho kimevuka daraja la tatu, hivyo nisingepnda kuona tena upo katika daraja la tatu. Katika wiki hii (na hata miezi kadhaa nyuma) nimekuwa mtu wa kushangaa vile unavyoandika Kiswahili safi na murua kuliko kile ninacho andika mie niliyezaliwa huku!! Je huoni hiyo sifa na faraja kubwa kumpita mwenye Lugha? Basi kila lakheri na hongera kwakuwa na Kiswahili bab-kubwa...--Mwanaharakati (talk) 16:20, 18 Februari 2008 (UTC)
Siku zote mtu hajijui bali hujuliwa!! Mie binafsi nimeona kiwango chako cha lugha ni cha juu kuliko, wewe unasema bado ni kidogo (sio kweli) kama unasema sentensi zako ni Kijerumani, mbona naona unaandika Kiswahili safi? Ama wewe mwenyewe hujiamini? Haifai kumvunja moyo mtu. Mimi kama mimi toka nije hapa nimetokea kukubali sana lugha yako wakati wa uhandishi (na hata maelekezo) yako yapo SUPERB, vipi wewe useme bado??? Basi sawa nimekuelewa!! Kazi njema...--Mwanaharakati (talk) 05:46, 19 Februari 2008 (UTC)
Salam. Naona hii sio hapa tu hata huko en:wiki na simple:wiki, pia kuna tatizo. Baada ya kucheza kwa template, kukawa na upotevu wa kifaa cha kufanyia kazi (REDIRECT button) sasa hakipo tena. Hicho hakipo katika wiki zote, sio sw:wiki, simple:wiki wala en:wiki. Nahisi ni msiba mkubwa kabisaaa... Katika en:wiki kulikuwa na vitufe kibao vya kufanyia kazi, lakini leo hii vimebaki kuwa sawa na vya sw:wiki!! Nilivyoona hivyo tu, nikagundua kwamba huu mtihani ni wa taifa zima la mradi wa wiki. Huenda wenyewe wakawa hawajui kama kuna tatizo kama hili. Huenda wakawa hawajui kama kuna mapungufu ya vitufe vya kufanyia kazi. Sasa tutafanyaje ndugu yangu? Maana habari ndio kama nilivyokeleza, tafakari!!..--Mwanaharakati (talk) 13:29, 19 Februari 2008 (UTC)
Unaweza kunielezea Hurricane kwa lugha nyingine mbali na Tufani? Nina mpango wa kutafsiri makala Hurricane Wilma na Hurricane Katrina, kwa maana ya Kimbunga cha Katrina na Kimbunga cha Wilma. Nikiandika neno "Kimbunga" kwa lengo la kupata maana zaidi ya moja naona sipati, inakuja hii moja tu ya Kimbunga lugha ya wabantu!! Sasa nifanyeje? Mimi nilikuwa sijui kama Kimbunga ni lugha. Nilikuwa najua Kimbunga ni upepo mkali unaotoka usawa wa bahari na kuelekea nchi kavu. Kuna kipindi kunaweza kukawa na Kimbunga wakati wa mvua nyingi ziambatanazo na upepo mkali, pia huwa tunaita Kimbunga. Je unalipi la kusema juu ya hili?--Mwanaharakati (talk) 13:46, 19 Februari 2008 (UTC)
Kimbunga ni lugha zoefu katika jamii yetu. Tufani ni jina geni sana midomoni mwa watu. Labda watu wa pwani wanaweza wakawa wanajua kama tufani ni kimbunga. Turahisishe: tuweke maana zaidi ya moja katika makala ya "Kimbunga" na mtu atakuwa na hiari yake ya kwenda katika makala ya Kimbunga (lugha) au katika Katrina-Wilma. Au waona vipi?--Mwanaharakati (talk) 06:00, 20 Februari 2008 (UTC)
Salam. Ndugu, ushapitia kule katika MetaWiki? Basi angalia majibu haya hapa...--"Mwanaharakati" (talk) 18:05, 20 Februari 2008 (UTC)
Hongera kwa kazi yako.. Tumejikwamua na tatizo hili la kucheza kwa template.. Una-stahili pongezi kwa kazi yako ulioifanya..--"Mwanaharakati" (talk) 05:47, 21 Februari 2008 (UTC)
Kipala, salam. Husika na kichwa cha habari hapo juu ni makala au kurasa ya kuelekeza, yaani, REDIRECT? Naona imetokea katika sehemu ya kurasa mpya!! Labda niulize ili nipate kujua, a)(b. Je ni sahihi ulivyoandika Ziwa Nyassa? Yaani, kwa-kuweka SSA badala ya SA tu. Nauliza tu, sijui lolote juu ya Nyasa au Nyassa!! Siku njema..----"Mwanaharakati" (talk) 11:13, 23 Februari 2008 (UTC)
Hiyo kurasa nimeikuta umeiandika: redirect halafu [[Ziwa Nyassa]], badala ya #REDIRECT kurasa... Basi kurasa haija-redirectiwa, badala yake imekuwa kurasa mpya!! Nilivyoona hivyo nikaweka zile alama za kuifanya kurasa ielekezwe kule sehemu husika!! Natumai umeelewa ama sivyo?--"Mwanaharakati" (talk) 11:44, 23 Februari 2008 (UTC)
Kipala, salam. Nimejaribu kumwuliza bwana Pathochilds kuhusu kuongeza baadhi ya vitufe katika wiki yetu. Hapo awali kulikuwa na vitufe kadhaa, lakini kwa sasa naona hamna. Jamaa akatoa ushauri wake namna ya kufanya ili vitufe virudi na vitaongezeka baadhi kama zilivyo wiki zingine zilizo kubwa. Katika jaribio hilo naona nilifeli kwakuwa jaribio la taka mtu aliyemkabidhi ndio afanye kazi hiyo!! Je unaweza ukapata kajimuda kidogo ili uweze kuifanya hiyo shughuli? Endapo utakuwa na muda, basi fungua hapa!! Siku njema.....--"Mwanaharakati" (talk) 12:04, 25 Februari 2008 (UTC)
Please excuse the English, but I do not know Swahili.
I would be happy to create a map of Tanzania. However, I am not quite sure what you want. I am not sure, for example, why you don't like the map that you marked up (the sketch that you showed me). Perhaps you could show me a map similar to what you would like to see, or more thoroughly describe it. Thanks, MapMaster 03:00, 28 Februari 2008 (UTC)
Rafiki yangu, nimekuteua uwe bureaucrat mwenzangu. Nimerudi nyumbani jana jioni tu baada ya wiki nne bila kuweza hata kuingia mtandaoni. Vizuizi hivyo havimsaidii bureaucrat. Tukiwa wawili tutasonga mbele vizuri zaidi. Wikipedia nyingi zina mabureaucrat wengi zaidi kuliko mmoja tu. Naomba msaada wako. Uangalie ukurasa wa wakabidhi. Asante, na ubarikiwe! --Oliver Stegen 09:22, 1 Machi 2008 (UTC)
Pole ukiwa na hisia ya kuadhibiwa. Haikuwa lengo langu. Kwa kweli nadhani unastahili, na bora kuwa wawili kuliko mmoja. Tusaidiane kazini :-) Nitasubiri siku chache ili kuwapa wengine nafasi ya kutoa maoni yao halafu nitakubureaucratisha. --Oliver Stegen 09:14, 5 Machi 2008 (UTC)
Salaam! Naomba tuendelee na jina la Category 'Waliofariki' mwaka fulani badala ya 'Waliokufa'. Asante! Wasalaam, --Oliver Stegen 18:42, 2 Machi 2008 (UTC)
Salam. Naam, nimeona tofauti kubwa baina ya sisi na wa yoruba. Ni kweli kabisa kwamba wao vimakala vyao vya kihuni. Haitoleta maana kama tutakaza mwendo wa kuandika makala fupi kama zile. Kuhusu filamu na muziki: Kusema kweli mimi sijui wanamuziki-waigizaji wengi wa nchi tofauti kuliko vile ninavyojua wa Kimarekani.
Maranyingi nikiwa naangalia filamu-muziki huwa naona tu watu na kuhifidhi majini yao kisha nakuja katika yahoo search na kuanza kumtafuta huyo niliyemuona amecheza vizuri na kuukonga moyo (bila kujua kama Mwamerika ama Mjerumani). Ikitokea huyo niliyemchagua akawa Mmarekani, basi sina budi kumwandika, awe Mswizaland Mwaustralia na wengine wote.
Tukienda mbele na kurudi nyuma, film industry zilizo-kubwa, nyingi zinatoka Marekani na ndiyomaana na shindwa kuapata waigizaji wengine waliowakali na wengi kuliko Marekani. Makala za msingi: Nikiangalia mule, naona nitaweza kumaliza wanamuziki wote na waigizaji pia.
Ni kiasai cha kutulia ili niweze kupambana na makala zile za waigizaji-wanamuziki. Shukrani: Ni vyema pia kukumbushana katika ujenzi huu wiki hii (namna ya kuandika na kufikia lengo), sikujisikia vibaya eti kwanini uliniambia niende katika ukuara wa makala za msingi la. Naona ni njia moja wapo ya kutaka kuikuza wiki yetu. Basi nashukuru kwa ujumbe wako!! Ubarikiwe!--"Mwanaharakati" (talk) 07:21, 3 Machi 2008 (UTC)
Hongera kwa kuchaguliwa kuwa mmoja wa mabureaucrat kwa wikipedia yetu ya Kiswahili. Sina wasiwasi yoyote kuhusu kufanya kazi pamoja nawe. Ukihitaji kumsajilisha mtumiaji kama akaunti ya kikaragosi, tumia ukurasa wa kumfanya mtumiaji awe bot. Kwa sasa sina shauri lingine. Haya, twende tukaendelee na kazi. Kila la kheri, --Oliver Stegen 18:49, 9 Machi 2008 (UTC)
Salam. Sijajua tatizo ni lipi. Sisi hatujafika huko katika sehemu ya kupakizia mafaili. Lakini ngoja niangalie mafuto maalum kisha nitakujibu..--Mwanaharakati (majadiliano) 14:15, 13 Machi 2008 (UTC)
Salam. Ndugu, nimejaribu kuielekeza Wikipedia:upload kwa Special:upload, lakini haelekei moja kwa moja. Inakwenda hadi katika kurasa husika kisha inasimama. Kwa-kuwa wote sasa tupo hewani, Oliver mie na wewe, ni vyema tutafakari namna ya kutatua tatizo hili. Unasemaje?--Mwanaharakati (majadiliano) 09:33, 15 Machi 2008 (UTC)
Samahani kidogo. Ninataka kuuliza swali. Hivi sasa ni saa ngapi huko kwenu? Ingaje swali laonekana kama si la msingi sana. Samahani lakini...--Mwanaharakati (majadiliano) 15:07, 15 Machi 2008 (UTC)
Hehe. Hata mimi nilifikiria hivyo kama itakuwa kwenye saa kumi hivi, ila nilikuwa nataka uhakika. Ahksante sana..--Mwanaharakati (majadiliano) 16:02, 15 Machi 2008 (UTC)
Hujambo bwana Kipala. Ninafurahi kupata nyayo zako na ninataka kukusalimu katika jina la Bwana na Mwokozi wangu Yesu Kristo. --213.219.135.57 16:11, 14 Machi 2008 (UTC)
Mimi ni Stefano Kaisavira, muzaliwa wa DR Congo. Kwa Kifaransa naitwa Etienne Kaisavira. Kiswahili ni lugha yangu tangu utoto. Na ninapendelea sana kuongea na watu katika hii lugha tukufu ya Kiswahili. Ninakaa hapa Brussels Belgium kwa muda wa zaidi ya miaka 12. Email yangu ni etienne.kaisavira@gmail.com na simu yangu ni +32474315897.--Stefano Kaisavira (majadiliano) 16:20, 14 Machi 2008 (UTC)
Sasa wewe unakaa wapi? Kwa Africa ama huku Ulaya? Namna gani ninaweza kukutana na wewe? Tafadhali, nitafurahi kupokea ujumbe wako katika email box yangu.--Stefano Kaisavira (majadiliano) 16:30, 14 Machi 2008 (UTC)
Salaaam! Naomba niulize kidooogo, maana huku kwetu Afrika bado hali ni tete katika teknolojia ya filamu. Swali ni hivi: Zile bastola wanazotumia katika kuigizia filamu ni za kweli? Na kama ni za uongo mbona zinatoa moto kama ulivyoelezea katika makala ya "Silaha za moto". Naomba nifumbue macho....--Mwanaharakati (majadiliano) 10:14, 18 Machi 2008 (UTC)
Sijaeleweka vizuri. Nauliza wakati pale mtu anapotumia silaha huku ndani yake kukiwa kuna ramia, mbona vitu huharibiwa? Inakuwaje!!! Au hii inaumiza....--Mwanaharakati (majadiliano) 14:07, 18 Machi 2008 (UTC)
Upo sahihi kabisa. Unaweza kutumia hata swichi, kwani hata huku pia huwa tunatumia swichi. Ukisema kiwashio, ni bora zaidi kwani utakuwa umetumia Kiswahili. Na ukisema Swichi, hapo inakuja ile kitu ya kusema unaandika neno la Kiingereza kwa maneno ya Kiswahili! Naona yote ni sawa tu. Na pia samahani kwa kuchelewa kukujibu swali lako... Kazi njema..--Mwanaharakati (majadiliano) 14:43, 19 Machi 2008 (UTC)
Bombom ni maneno ya kizamani sana. Tumia "Bomu". Kiwashio: Ni sawa kabisa kwamba ni "kidude kinachowashia ramia" hili liko sawa wala usitie shaka. Kuna la zaidi?--Mwanaharakati (majadiliano) 16:07, 19 Machi 2008 (UTC)
Ndugu, nimegundua jamii mbili ambako moja ingetosha - angalia majadiliano ya ukurasa wa jamii hii. Pole na usumbufu! Nitasubiri oni lako kabla sijasawazisha hizo mbili ziwe moja. Asante! --Oliver Stegen (majadiliano) 21:05, 22 Machi 2008 (UTC)
Heheh. Nilikuwa nikiita "makala" lakini za katika televisheni, hapo je?--Mwanaharakati (majadiliano) 09:36, 25 Machi 2008 (UTC)
Mambo vipi! Mkubwa, naomba umwelezee kwa kirefu "Mzungu" (na hata kutaja asili ya wazungu) maana mie nimejaribu kuelezea kidogo tu. Sasa naomba uchungue makala ile ya Mzungu! Nitashukuru kama utapata kajimuda hiko, Wasalaam,--Mwanaharakati (majadiliano) 14:18, 25 Machi 2008 (UTC)
Salaam! Naona mkubwa umekuja kwa mkwala mzito kabisaa (Usidharau kamusi tena!) Furaha teeele! Sawa mkubwa wangu. Ila nasikitika kwa kukosa kukuona tena kama awali. Hata hivyo katika wiki hizi moja-mbili naona ulikimbiza ajabu. Mimi nipo kama mlinzi katika wiki yetu! Mara nyingi huwa naangalia "mabadiliko ya karibuni" na kujua mengi yaliyojiri katika wiki hii! Basi kila lakheri mkubwa wangu. Kingine: Waweza kufuatilia habari za Checkuser? Hapa kwetu naona hamna checkuser na sisi pia twaitaji checkuser. Tafadhali naomba ufuatilie hili kama inawezekana!--Mwanaharakati (majadiliano) 10:01, 26 Machi 2008 (UTC)
Salaam. Kuna kajimchezo nataka nikajue jina lake kanaitwaje. Niliona katika TV wakionyesha Wazungu wa Ulaya wakicheza mchezo wa kupigiza viatu huku wakiwa wanalukaluka, yaani wanavyocheza viatu ndiyo vinasikika sana kuliko chochote katika mchezo huo. Je huo mchezo unaitwaje?--Mwanaharakati (majadiliano) 11:55, 31 Machi 2008 (UTC)
Kuna ngoma kadhaa zinavyochezwa hivyo. Nchi mbalimbali. Kama wanapiga mapaja pia ni Wabavaria kutoka kwetu kusini au majirani Waaustria. Wengine ni Wahispania. Ukiangalia picha hizi utaona vikundi vinavyocheza ngoma za kienyeji sehemu mbalimbali. Kama wamevaa kiutamaduni ni rahisi zaidi kusema ilikuwa nini. --Kipala (majadiliano) 13:08, 31 Machi 2008 (UTC)
Salam. Kuna neno nimeshindwa kutafsiri. Naomba nisaidie maanake halisi:
Wakati najaribu kuandika makala ya César Cui. Naomba nisaidie!--Mwanaharakati (majadiliano) 09:29, 3 Aprili 2008 (UTC)
Salam. Hapa sipati picha iliyo kamili. Labda uiite "Jamii za nafaka" kwani kunde hutaja jina moja tu! Kunde ni kunde tu kama kunde. Na kunde ipo ndani ya nafaka, nafaka ni maharagwe, njegele, njugumawe, dengu, choloko na kadhalika. Jaribu kutunga jina lolote lile la kutaja vitu hivyo vyote mbali na "Jamii kunde". Unaonaje?--Mwanaharakati (majadiliano) 12:00, 5 Aprili 2008 (UTC)
Kingine kuhusu "mboga" ni "vegetable". Hapa nimeona tangu muda mrefu kamusi zinataja mboga lakini watu huwa na maana pana zaidi ndani ya mboga ama majani ama nyama. Sijui yale yanaoitwa vegetable unaita nini? --Kipala (majadiliano) 13:19, 5 Aprili 2008 (UTC)
Salama nyingi zikufikie Nd. Kipala. Nilikuwa naomba msaada wa kutafsri baadhi ya maneno kutoka hapa, nitashukuru kama utanipatia msaada huo! Kazi njema....--Mwanaharakati (majadiliano) 06:58, 14 Aprili 2008 (UTC)
Salam. Mkubwa samahani kidogo. Naona kuna tatizo la kuelekea katika ukurasa wa mwanzo, yaani ile logo yenye kuonyesha kama hii ni Wikipedia (Kamusi elezo huru) naona hakuna na badala yake imekaa picha ya askari wa doria. Je ni mimi tu ndiyo ninayoona hivyo au hata wewe mwenzangu waona hivyo?--Mwanaharakati (majadiliano) 15:07, 16 Aprili 2008 (UTC)
Sasa huyo askari anafanya nini katika hiyo sehemu ya logo ama kwako huoni?--Mwanaharakati (majadiliano) 15:30, 16 Aprili 2008 (UTC)
Navuta subira huenda na kwako ikawa! Na mara itakapofika kwako ndiyo tutachukua hatua lakini kwa sasa bado ni mapema mno. Au wewe unaonaje nikifanya subra kwanza....--Mwanaharakati (majadiliano) 05:49, 17 Aprili 2008 (UTC)
Salam. Naona isharudi kama awali. Vipi umefanya maarifa? a)(b Piano kumbe ni nini kama sio Kinanda?--Mwanaharakati (majadiliano) 06:45, 18 Aprili 2008 (UTC)
Ahsante kwa ushauri wako. Lakini kulikuwa na tatizo la kuingiliana kwa IP address yetu na mtu mwingine, yaani IP moja tunatumia watu wawili hivyo ilileta mgogoro. Lakini kwa sasa wesha weka sawa! Kuhusu piano: Hapa bado naona kizungumkuti kabisaa, organ, piano na keybord. Labda nikupe tofauti ndogo:
1. Piano: mara nyingi tunaamini kwamba ni kinanda kile cha Kanisani (hasa wakatoliki) na kile cha Wazungu wanachoweka majumbani mwao!
2. Organ: ni kinanda cha wapiga taarab, yaani hutumia kupiga kwa kushika mkononi huku akiwa wima. Ni hasa wale wapigaji wa kale (zilipendwa)
3. Keybord: ni kinanda cha wapiga muziki wa kawaida, yaani wapiga muziki wa taarab, mabendi, makanisa ya kilokole n.k.
Pamoja na kuwa na mlolongo mrefu wa maelezo kuhusiana na hayao, lakini bado vyote tunaviita vinanda bila kubagua namna vilivyo! Unaonaje?--Mwanaharakati (majadiliano) 08:42, 18 Aprili 2008 (UTC)
Kipala na Oliver, hongereeni kwa kusukuma wiki yetu juu ya kiwango cha makala 7,000! Nafurahia kuona tumefikia makala elfu saba. Naona kama naota kufikia kiwango hicho, ingawaje si nyingi hivyo lakini tumefika!. Basi tuendelee kushauriana na kuvumiliana!--Mwanaharakati (majadiliano) 07:28, 21 Aprili 2008 (UTC)
Ndugu Kipala, asante kwa mawasiliano. Nakubali kichwa Ualimu kibadilishwe kiwe Ualimu wa Kanisa, ila sijui namna ya kukibadilisha... Pia ningependa Klara kiwe Klara wa Asizi. Fanya wewe!