Moto mkubwa.
Pembetatu ya moto inaonyesha masharti matatu yanayohitajika kwa moto kuwaka.
Kiberiti kinawaka.

Moto ni hali ya kuungua haraka kwa gimba na kutoa joto pamoja na nuru. Kisayansi ni mmenyuko wa kikemia kati ya oksijeni ya hewani na kampaundi za kaboni. Moto ni mfano mkuu wa harakati ya kuoksidisha.

Katika historia ya binadamu matumizi ya moto yalikuwa hatua kubwa ya kujenga utamaduni. Watu hutumia moto kwa kupika, kujilinda dhidi ya baridi na giza, kupeana habari, kuendesha vyombo vya usafiri na kutengeneza umeme.

Moto ni pia jambo haribifuː unaleta hatari kwa mali, afya na maisha ya watu na viumbe vyote.

Moto kikemia

Moto inawaka kama masharti manne yako mahali pamoja:

Masharti haya manne huelezwa kwa tetrahedroni ya moto. Hakuna moto kama masharti hayo manne hayapo pamoja.

Mmenyuko mfululizo ni lazima kwa kuendelea kwa moto ukihkikisha ya kwamba kuna joto la kutosha kuendeleza moto.

Moto inazimika kama moja kati ya masharti manne linaondolewa. Katika mfamo wa moto ya gesi kwenye jiko la kupikia ya gesi moto huu unazimika kwa:

Moto na utamaduni

Mtu akikoleza moto kiasili

Matumizi asilia ya moto

Wataalamu wanaamini ya kwamba watu wa kale sana waliona faida ya kutumia moto uliotokea kiasili kutokana na radi n.k. Walipokuta wanyama waliokufa katika moto wa aina hii waliona ya kwamba nyama iliyochomwa na moto ni lishe bora kuliko nyama mbichi. Walitambua pia ya kwamba mimea au sehemu za mimea zilikuwa chakula bora baada ya kukaa motoni kwa muda fulani.

Kwa hiyo inaaminiwa watu kama hao kwanza walijifunza kubeba moto asilia na kuutunza kwenye makazi yao, baadaye walijifunza kuwasha moto. Kuwa na moto karibu na makazi au mahali pa kulala kulikuwa namna ya ulinzi dhidi ya wanyama wakali wanaoogopa moto na hawana akili ya kubainisha matumizi yake. Moto ulisaidia pia wakati wa kuwinda.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Moto kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.