Mkoko | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Mkoko magondi (Rhizophora mucronata)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Mikoko ni aina za miti au vichaka vinavyokua katika maji ya chumvi kwenye fuko za bahari za kanda za tropiki[1]. Miti hii inaainishwa katika jenasi tatu: Bruguiera, Ceriops na Rhizophora katika familia Rhizophoraceae. Pengine jina hili hutumika kwa Theobroma cacao lakini afadhali jina mkakao litumike kwa mti huu.
Takriban 1/3 ya pwani kwenye tropiki huwa na mikoko au miti ingine inayoweza kukua katika maji ya chumvi[2]. Msitu wa mikoko huitwa kapa au wangwa.
Mizizi ya mikoko inaweza kushika matope na hivyo husaidia kukinga pwani na kujenga visiwa.
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkoko kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |