Ramani inayoonyesha halijoto wastani ya uso wa bahari. Ramani za aina hii ni tokeo ya miaka mingi ya vipimo na pia msaada muhimu kwa kuelewa utaratibu wa mabadiliko ya halihewa kama kutokea kwa dhoruba au kunyesha au kutonyesha kwa mvua

Metorolojia (kutoka Kigiriki μετεωρολογία, meteorologia; kwa Kiingereza meteorology) ni sayansi inayoshughulikia habari za angahewa, tabianchi na halihewa na hasa fizikia pamoja na kemia husika.

Tabia za angahewa

Tabia za msingi za halihewa ni mwendo wa upepo, halijoto, umawingu, unyevu, kanieneo, kiwango cha mnururisho wa jua, uvukizaji na nyingine. Tangu karne nyingi wataalamu wamejitahidi kupima tabia mbalimbali za halihewa na angahewa kama msaada wa kuzielewa vizuri zaidi na kujenga msingi kwa utabiri wake.

Vifaa vya metorolojia

Metorolojia imeanza kutokea kadiri wataalamu walivyoanza kuchukua vipimo halisi vya tabia za angahewa na kuvilinganisha. Mwelekeo huo ulileta kubuniwa kwa vifaa vya upimaji maalumu vinavyounganishwa kwenye vituo vya metorolojia. Data kutoka vifaa hivyo zinatunzwa kwa muda mrefu, zinaruhusu kutabiri halihewa na kuangalia mabadiliko ya tabianchi.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Metorolojia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.