Mango (wakati mwingine pia: yabisi[1]) ni moja kati ya hali maada. Maana yake ni imara, tofauti na kiowevu (majimaji) au gesi (kama hewa).
Katika hali mango atomu zinakaa mahali pamoja katika gimba, hazichezi wala kusogea ndani yake. Kila atomu ina mahali pake. Gimba mango lina umbo, mjao na uzani maalumu. Umbo mango lina urefu, upana na kimo chake, tofauti na kiowevu kinachobadilika umbo kufuatana na chombo chake au gesi isiyo na umbo wala mjao maalumu.
Kama mango inabadilika kuwa kiowevu tunasema inayeyuka. Kama inabadilika kuwa gesi au mvuke moja kwa moja tunaliita badiliko hili mvukemango.
Maana ya asili ya "mango" ni jiwe gumu jeusi lililotumika kutwanga kumetesha au kukatua kitu. [2]
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mango kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |