Kidole cha shahada
Majina ya vidole vya mkono:
1 Kidole gumba, 2 Kidole cha shahada,
3 Kidole kirefu, 4 Kidole cha pete, 5 Kidole cha mwisho

Kidole cha shahada ni kidole cha pili mkononi. Iko kati ya kidole gumba na kidole kikubwa. Kidole hiki kinatumiwa sana kwa mawasiliano kati ya watu.

Kwanza hutumiwa kwa kukilenga kwa kitu kwa kwa mtu kwa kusudi la kumaanisha: Ndiye huyu, ndicho hiki! Pia kinadokeza mweleko au upande. Kwa lugha mbalimbali jina la kidole hiki ni "kidole cha kuonyesha" (kiing. index au pointer finger, kijer. Zeigefinger).

Matumizi mazuri hutegemea na utamaduni.


Sehemu za Mkono wa binadamu

Bega * Mkono wa juu * Kisugudi * Kigasha * Kiganja * Kidole gumba * Kidole cha shahada * Kidole cha kati * Kidole cha pete * Kidole cha mwisho