Kidenenda | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kidenenda mvivu
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 2: |
Videnenda ni ndege wadogo wa jenasi Cisticola na Incana katika familia Cisticolidae. Chimbuko la jenasi lipo Afrika lakini spishi kadhaa zinatokea Ulaya na Asia pia, spishi moja hata mpaka Australia. Ndege hawa hupatikana kwa maeneo wazi, k.m. savana, jangwa, mbuga na mabwawa. Rangi yao kuu ni kahawia mara nyingi pamoja na michirizi mizito na pengine nyekundu au njano. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe ndani ya uoto mzito; mara nyingi tago limefunika na manyasi yaliyofumika. Jike huyataga mayai 3-5.