Josephs Quartzy | |
---|---|
Amezaliwa | Joseph Marwa 16 Aprili 1999 Musoma vijijini Tanzania |
Kazi yake | Mwigizaji Mwimbaji Mwandishi |
Joseph Quartzy (amezaliwa 16 Aprili 1999) ni mwigizaji, mwimbaji na mwandishi kutoka Tanzania. Anajulikana zaidi kwa kucheza Nhwale katika filamu ya mapenzi ya mwaka 2019 Mr Local Man na kwa kuigiza Josephs katika mfululizo wa tamthilia ya mwaka 2021 JQ Knew That. Yeye ni mwanachama wa kundi la muziki la The Eastern Bandits. Joseph Quartzy anaandaa kipindi cha mazungumzo cha BTN, The Real Past Show ambacho amekiandaa kwa misimu mitatu sasa.
Kama mwandishi, Josephs Quartzy[1] alianza kazi yake ya uandishi mnamo 2018 wakati bado alikuwa mwanafunzi wa shule ya upili(sekondari), akiandika vitabu kama vile New People in Codes, The World of Philosophy, Life's Telescope, na Malaika aliyepotea ambavyo havikufanya vizuri sokoni kwa sababu havikuwahi kuchapishwa wala kukaguliwa kwa viwango bora[2]. Mapema mwaka 2022, Josephs alishirikiana na mchapishaji na msambazaji kutoka India wakati aliweza kuandaa na kuchapisha vitabu kwa ubora wa juu. Josephs anaandika zaidi kuhusu masimulizi ya kufikirika kulingana na aina za hadithi za jumla, ingawa pia ameshughulikia aina za mapenzi,Filosofia pia tamthilia za kutisha[3].
Mwaka | Jina | Mchapaji | ISBN |
---|---|---|---|
2022 | A Tale of an Intelligent Psychopath: Based on a True story | Pencil Publishers | ISBN 978-93-56104-98-3 |
2022 | Irene: The Andromeda | Pencil Publishers | ISBN 978-93-56105-84-3 |
2022 | A Blessed Curse | Pencil Publishers | ISBN 978-93-56670-88-4 |
Hizi ni filamu ambazo mwigizaji Josephs Quartzy ameshiriki[4]
Mwaka | Filamu | Uhusika |
---|---|---|
2019 | Mr. Local Man | Nhwale |
2020 | Lucifer'e and the great Controversy | Angeljoe |
2019 | Africa | Ngowi |
2019 | NIGGA | Dos |
2020 | Not so different | Mwenyewe |
2022 | Homeboy Never Fails | Ghetto boy/Yale |
Hizi ni Tamthilia ambazo Josephs Quartzy ameshiriki[5]
Mwaka | Jina | Uhusika | Maelezo |
---|---|---|---|
Tangu 2019 | The Real Past show | Mtangazaji | |
2021-2022 | JQ Knew That | Josephs | |
2021 | Big Brother-Nagwa | neighbour | sehemu ya kwanza |