Jiografia ya Afrika inahusu bara hilo ambalo ni la pili duniani kwa ukubwa, likiwa na eneo la kilometa za mraba zipatazo 30,368,609 (6% za eneo lote la dunia, sawa na 20% za nchi kavu) na vilevile kwa idadi ya wakazi, hao wakiwa 1,275,920,972 (mwaka 2018). Asia ndiyo bara pekee la kushinda Afrika.
Kuna umbali wa kilomita 8,000 kutoka Ras ben Sakka nchini Tunisia (37°21' N, sehemu ya kaskazini kabisa) hadi rasi ya Cape Agulhas nchini Afrika Kusini (34°51'15" S, sehemu ya kusini kabisa)[2] .
Umbali ni km 7,400 kutoka upande wa magharibi (rasi ya Cape Verde, 17°33'22" W) hadi mashariki (Ras Hafun nchini Somalia, 51°27'52" E)[3].
Mlima mrefu zaidi barani unapatikana nchini Tanzania: ni volkeno Kilimanjaro (mita 5,895 juu ya usawa wa bahari) ambao ni pia mlima mrefu kuliko yote duniani usiojitokeza katika safu ya milima.
Mto mrefu zaidi barani na duniani ni Naili ukiwa na mwendo wa kilometa 6,758 kuanzia nchini Rwanda na Burundi, kupitia Tanzania, Uganda, Kenya, Sudan Kusini, Ethiopia, Sudan na hatimaye Misri.
Katika mwendo wake wa awali maji ya Naili yanakusanyika katika ziwa Nyanza/Viktoria ambalo ni pana kuliko yote barani na la pili duniani likiwa na kilometa mraba 59,947.
Afrika imezungukwa na bahari karibu pande zote. Kuna kiungo chembamba cha nchi kavu upande wa kaskazini mashariki na bara la Asia kwenye rasi ya Sinai [4].
Upande wa kaskazini iko Bahari ya Mediteranea, upande wa mashariki kuna Bahari Hindi pamoja na Bahari ya Shamu na upande wa magharibi iko Bahari Atlantiki.
Pwani yote ya Afrika ina urefu wa kilomita 26,000.
Kuna kisiwa kikubwa cha Madagaska na funguvisiwa mbalimbali.
Kijiolojia Afrika iko kwenye bamba la Afrika. Lile bamba la gandunia la Afrika linaenea mbali zaidi kuliko maeneo tunayotazama kuwa Afrika kijiografia, ni pamoja na maeneo chini ya bahari linapopakana na mabamba ya Ulaya-Asia, Uarabuni, Uhindi na Australia, Antaktika, Amerika ya Kusini na Kaskazini. Upande wa mashariki wa bamba la Afrika kuna ufa unaozidi kupanuka ikielekea kujitenga kutoka Afrika kama bamba la Somalia.
Tabianchi ya Afrika ni pana, kuanzia kanda za tropiki hadi kufikia maeneo ya nusu-aktiki (baridi) kwenye ncha za milima mirefu.
Nusu ya kaskazini ya bara ni jangwa au angalau yabisi. Sehemu za kati na za kusini zina maeneo ya savanna na kanda za msitu wa mvua.
Afrika ni bara lenye joto kuliko mabara yote na asilimia 60 za uso wake ni maeneo yabisi au jangwa. [5]
Barani kuna nchi huru 54 zinazotambuliwa na Umoja wa Mataifa, maeneo 9 yenye hali ya pekee na madola mawili ambayo yanajitawala bila kutambuliwa kimataifa.
Nchi kubwa ya Afrika ni Algeria na nchi ndogo ni Shelisheli, funguvisiwa la Bahari Hindi.[6] Nchi ndogo Afrika bara ni Gambia.
Wataalamu wengi wanakubaliana kutambua Afrika kama asili ya binadamu wote walioko duniani. [7]
Mwaka 2010 idadi ya wakazi wa nchi zote za Afrika ilipita bilioni 1. Ni kwamba idadi yao imeongezeka sana katika miaka 40 iliyopita, ikipiku zile za Ulaya na Amerika.
Ilhali mwaka 1950 walikuwepo Waafrika milioni 229 pekee, idadi iliongezeka kuwa milioni 630 mwaka 1990 na milioni 1200 mnamo 2014. [8] [9]
Hivyo asilimia ya watoto na vijana ni kubwa. Kuna nchi kadhaa ambako zaidi ya nusu ya wananchi wako chini ya umri wa miaka 25.[10] Wakazi wa Afrika ni vijana kuliko wale wa mabara mengine yote;[11][12] mwaka 2012 umri wa wastani ulikuwa miaka 19.7, wakati kidunia ulikuwa 30.4.[13]
Zaidi ya lugha elfu za Kiafrika zinazungumzwa barani leo, ingawa nyingi zinazidi kufifia.
Waafrika wana imani za dini nyingi tofauti, lakini takwimu zinazotolewa hazina hakika, pia kwa sababu suala hilo ni nyeti kisiasa kwa serikali zenye mchanganyiko mkubwa wa watu, kama vile Nigeria, Ethiopia na Tanzania.[14][15]
Kadiri ya World Book Encyclopedia, Islam ndiyo inayoongoza, ikifuatwa na Ukristo. Kumbe kadiri ya Encyclopedia Britannica, 45% za wakazi ni Wakristo, 40% ni Waislamu na 10% wanafuata dini asilia za Kiafrika. Wachache tu ni Wahindu, Wabuddha, Wabaha'i au hawana dini yoyote.
((cite web))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
((cite web))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Mada za Afrika | |
---|---|
Jiografia | |
Historia | Homo · Historia ya awali · Wawindaji-wakusanyaji · Ujima · Misri ya Kale · Uenezi wa Kibantu · Uenezi wa Uislamu Afrika · Falme za Afrika kabla ya ukoloni · Biashara ya watumwa · Biashara ya utumwa kupitia Bahari ya Hindi · Biashara ya utumwa kupitia Atlantiki · Biashara ya ng'ambo ya Sahara · Ukomeshaji wa Biashara ya Watumwa · Historia ya uchumi · Upelelezi wa Wazungu Afrika · Ukoloni Afrika · Mkutano wa Berlin wa 1885 · Muungano wa Afrika · Uhuru · Ukoloni mamboleo Afrika · Vita na migogoro) · Maafa |
Siasa | Haki za binadamu · Matabaka · Vyombo vya habari · Vyama vya siasa · Chaguzi · Watawala wa Afrika · Umoja wa Afrika · Bunge la Umoja wa Afrika |
Demografia | Majiji · Miji · Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu · Uhamaji · Uhamiaji · Ukimwi · Makabila ya Afrika |
Uchumi | Maliasili ya Afrika · Orodha ya nchi za Afrika kwa GDP · Orodha ya nchi za Afrika kwa HDI · Benki kuu · Sarafu · Masoko ya hisa · Miundombinu · Nishati mbadala · Wavuti · Afya · Ufukara Afrika |
Utamaduni wa Kiafrika | Falsafa · Dini · Fasihi ya Kiafrika (Orodha ya Waandishi katika nchi za Afrika) · Itifaki · Lugha · Elimu · Muziki · Sanaa · Sinema · Usanifu majengo · Urithi wa Dunia · Mapishi |
Michezo | African Cricket Association · Afro-Asian Games · Michezo ya Afrika Nzima · Confederation of African Football (Kombe la Mataifa ya Afrika) · Confederation of African Rugby (Africa Cup) · FIBA Africa · Viwanja vya michezo · Tour d'Afrique |
Book |