James Omingo Magara ni mwanasiasa wa Kenya. Kwa sasa ni mwanachama wa Orange Democratic Movement na alichaguliwa kuwa mbunge wa Mugirango Kusini katika uchaguzi wa 2007.
Alishinda kiti hiki mara ya kwanza kwa tiketi ya FORD-Kenya katika uchaguzi mdogo mnamo 2001, akichukua nafasi ya nduguye Enock Nyakieya Magara aliyefariki katika ajali ya gari.
Alihifadhi kiti chake katika Uchaguzi mkuu wa Kenya wa 2002, wakati huu akiwakilisha chama cha Ford People na pia katika Uchaguzi wa 2007, akiwakilisha Chama cha ODM[1]
Tangu kuchaguliwa amewahi kuwa Naibu wa Waziri wa biashara. Hata hivyo, mnamo Desemba,2009, Mahakama kuu ya Kenya ilitangaza kiti cha Ubunge cha Mugirango Kusini wazi kutokana na udanganyifu katika uchaguzi, ingawa Magara mwenyewe hakupatikana na hatia ya udanganyifu[2]
Makala hii kuhusu mwanasiasa huyo wa Kenya bado ni mbegu. Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |