Mchanganyiko wa familia ya Kihawai / Ulaya na Amerika huko Honolulu, 1860s








Hawaii

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Marekani Marekani
Mji mkuu Honolulu
Eneo
 - Jumla 28,311 km²
 - Kavu 16,635 km² 
 - Maji 11,677 km² 
Tovuti:  http://www.hawaii.gov/
Ramani ya Hawaii

Hawaii (kwa Kihawaii: Mokuʻāina o Hawaiʻi) ni funguvisiwa la bahari ya Pasifiki ambalo ni jimbo la Marekani, pia ni jina la kisiwa chake kikubwa.

Hawaii ilikuwa ufalme wa Wapolinesia, ikawa koloni la Marekani]] katika karne ya 19 na imekuwa jimbo la Marekani tangu tarehe 21 Agosti 1959.

Mji mkuu ni Honolulu kwenye kisiwa cha Oahu.

Jiografia

Funguvisiwa la Hawaii lina jumla ya visiwa 137 vyenye eneo la kilomita za mraba 16,649 za nchi kavu. Visiwa vilivyo vingi ni vidogo, havikaliwi na watu.

Visiwa vikubwa, kuanzia magharibi kwenda mashariki, ni:

Visiwa vyote vina asili ya kivolkeno. Mlima Mauna Kea ni volkeno ndefu kabisa duniani yenye kimo cha mita 4201 juu ya UB lakini inaanza chini ya bahari katika kina cha mita 5,000, hivyo kimo cha jumla ni zaidi ya mita 9,000. Volkeno ya pili ni Mauna Loa yenye masi kubwa zaidi. Mauna Loa ni volkeno hai kwenye kisiwa kikuu cha Hawaii, pamoja na mlima Kilauea.

Historia

Hawaii ilikaliwa na Wapolynesia waliofika kwa mitumbwi yao mikubwa. Jamii zao zilitawaliwa na familia za makabaila zilizotazamiwa kuwa za juu kuliko watu wa kawaida. Tabaka la pili la juu lilikuwa lile la makuhani.

Kati ya miaka 1781 na 1811 Kamehameha I alifaulu kuunganisha visiwa vyote chini ya utawala wake akawa mfalme wa kwanza wa Hawaii yote.

Katika miaka ya karne ya 19 iliyofuata wageni kutoka Marekani na Ulaya walianza kujenga makazi visiwani. Uchumi wa kisasa ulianzishwa kwa mashamba ya miwa na uvuvi.

Mwaka wa 1842 Marekani ikatambua ufalme wa Hawaii kama nchi huru ya kujitegemea.

Athira ya wafanyabiashara matajiri Wazungu ikakua. Kwa njia ya ghasia wakamlazimisha mfalme Kalakaua mwaka 1887 kukubali katiba iliyowapa haki ya kupiga kura matajiri pekee. Mwaka uleule Marekani ilipewa haki ya kutawala kituo cha kijeshi cha Pearl Harbour.

Malkia Liliuokalani († 1917) alijaribu mwaka 1893 kufuta katiba na kurudisha mamlaka ya wafalme lakini alipinduliwa na wenye mashamba makubwa waliosaidiwa na wanajeshi wa Marekani, na jamhuri ya Hawaii ikatangazwa.

Wakati wa Vita ya Marekani dhidi Hispania serikali ya Marekani iliamua kutwaa Hawaii na kuitangaza kuwa mali ya Marekani. Baadaye visiwa vilitawaliwa kama koloni na baadaye kama eneo la kitaifa la Marekani.

Marekani iliingia katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia kwa shambulio la Japani dhidi ya manowari za Marekani katika bandari ya Pearl Harbour tarehe 7 Desemba 1941.

Tarehe 21 Agosti 1959 Hawaii imekuwa jimbo kamili la Marekani.

Watu

Wakazi wake ni 1,419,561 (2014), kati yao 10% ni Wahawaii asili; wengi zaidi ni Wazungu, machotara wa aina mbalimbali, Wafilipino, Wajapani n.k.

Lugha rasmi ni Kiingereza, inayozungumwa nyumbani na 75% ya wakazi, na Kihawaii.

Upande wa dini, wengi ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, kuanzia Kanisa Katoliki, likifuatwa na Wamormoni. Lakini Waprotestanti kwa jumla ni wengi zaidi.

Picha

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Hawaii


Majimbo ya Marekani

AlabamaAlaskaArizonaArkansasCaliforniaColoradoConnecticutDelawareFloridaGeorgiaHawaiiIdahoIllinoisIndianaIowaKansasKentuckyLouisianaMaineMarylandMassachusettsMichiganMinnesotaMississippiMissouriMontanaNebraskaNevadaNew HampshireNew JerseyNew MexicoNew YorkNorth CarolinaNorth DakotaOhioOklahomaOregonPennsylvaniaRhode IslandSouth CarolinaSouth DakotaTennesseeTexasUtahVermontVirginiaWashingtonWest VirginiaWisconsinWyoming


Nchi_na maeneo ya Australia na Pasifiki
Australia | Fiji | Guam | Hawaii | Kaledonia Mpya | Kiribati | Kisiwa cha Pasaka | Mikronesia | Nauru | Nyuzilandi | Niue | Pitcairn | Polinesia ya Kifaransa | Palau | Papua Guinea Mpya | Samoa | Samoa ya Marekani | Visiwa vya Cook | Visiwa vya Mariana ya Kaskazini | Visiwa vya Marshall | Visiwa vya Solomon | Tonga | Tuvalu | Vanuatu | Wallis na Futuna
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hawaii kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.