Gang Starr
DJ Premier na Guru
Maelezo ya awali
Asili yake Boston, Massachusetts
Brooklyn, New York
Aina ya muziki Hip hop
Jazz rap
Alternative hip hop
Miaka ya kazi 1987 - 2005
Studio Wild Pitch
Chrysalis
Noo Trybe Records
Virgin
Ame/Wameshirikiana na Gang Starr Foundation
Wanachama wa zamani
Guru
DJ Premier
Gang Starr (1999)

Gang Starr lilikuwa kundi la muziki wa hip hop lenye athira kubwa ya East Coast hip hop. Kundi linaunganisha watu wawili, ambao ni MC Guru na DJ/mtayarishaji DJ Premier. Kundi hilo lilijulikana sana kwa staili ya aina yao, ambayo inajumlisha baadhi ya elementi za hip hop na swing jazz ya New York.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kundi lilianzishwa mnamo mwaka wa 1986 na Guru (baadaye akaja kujulikana kama Keithy E. The Guru) na DJ 1,2 B-Down (pia anajulikana kama Mike Dee) na watayarishaji kadhaa, kama vile Donald D, J.V. Johnson au DJ Mark the 45 King naye alisaidia kuanzishwa kwa kundi hili. Mnamo 1987 na 1988, Gang Starr wakatoa single ya kwanza iliyofanyika katika studio za Wild Pitch label.

Mnamo 1989, kundi likasambaratika na wanachama pekee waliotaka kuliendeleza kundi wakapendekeza jina la Gang Starr, na huyo alikuwa Guru. Baadaye akapata kuwasiliana na DJ Premier (baadaye akajakujulikana kama Waxmaster C) ambaye alimtumia tepu ya biti iliyompendeza Guru. Baada ya kuipata biti, akaona bora amwalike DJ Premier ili aungane na Gang Starr na katika mwaka huohuo wakatoa single yao iliyokwenda kwa jina la "Words I Manifest" ikiwa sambamba na albamu iliyopewa jina la "No More Mr. Nice Guy" (1989).

Wakati wa shughuli zao Gang Starr walisaidia kuvumbua sauti ya hip hop ya New York. Matoleo yote ya Gang Starr, hasa Step in the Arena (1991), Daily Operation (1992) "Hard to Earn" (1994) na Moment of Truth (1998) zilipata heshima kubwa saana. Wimbo wa "Jazz Thing", uliokuwemo kwenye filamu ya Spike Lee ya Mo' Better Blues, ilisaidia kuinua sauti ya jazz rap.

Gang Starr Foundation

[hariri | hariri chanzo]

Hali ya sasa

[hariri | hariri chanzo]

Discografia

[hariri | hariri chanzo]

Marejeo

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "UKMIX - Forums - View topic - SoundScan Era - USA's Best Selling Artists and Albums". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-06-21. Iliwekwa mnamo 2009-05-26.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]