Friedrich Wilhelm Nietszche

Friedrich Wilhelm Nietzsche (tamka: nits-she; 15 Oktoba 1844 - 25 Agosti 1900) alikuwa mwandishi na mwanafalsafa kutoka Ujerumani.

Maisha

Alikuwa mtoto wa mchungaji wa Kiluteri akaendelea kusoma lugha za kale za Kilatini na Kigiriki akawa profesa wa lugha za kale kenye chuo kikuu cha Basel. 1879 alipaswa kujiuzulu kutokana na matataizo ya kiafya na tangu 1889 alionyesha dalili za ugonjwa wa akili akaendelea kutunzwa na mama na dadake hadi kifo chake 1900.

Maandishi

Nietzsche amejulikana kama mwanafalsafa aliyepinga mawazo ya wakati wake na hasa Ukristo. Huhesabiwa kati ya wapizani wa dini kwa ujumla. Akiwa kijana aliathiriwa na mwanafalsafa Schopenhauer pamoja na muziki ya Richard Wagner.

Alipenda sentensi fupi-fupi na sehemu ya kazi zake ni mkusanyiko wa sentensi hizo.

Alitangaza kifo cha Mungu aliyemwona kama dhana ya kibinadamu tu iliyopitishwa na wakati akitabiri ya kwamba kumwaga Mungu kutaleta mvurugu mwingi kwa utamaduni. Badala yake alitangaza kuja kwa "mwanadamu wa juu".

Kati ya vitabu vyake ni:

Maneno kadhaa