Faiza Darkhani (alizaliwa 1992) ni mwalimu, mwanamazingira na mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Afghanistan.[1] Mnamo mwaka 2021, alitajwa katika orodha ya wanawake 100 ya BBC inayojumuisha majina ya wanawake wenye ushawishi mkubwa duniani.[2] Darkhani ni miongoni mwa wasomi wachache waliopata elimu ya sayansi ya tabianchi huko Afghanistan.[2] Pia alikuwa mkurugenzi kwenye Shirika la Taifa la Kulinda Mazingira katika jimbo la Badakhshan, Afghanistan.[1]
Alisoma chuo kikuu cha Badakhshan pamoja na chuo kikuu cha Putra Malaysia na kupata shahada ya uzamili ya sanyansi katika usanifu wa mazingira.[1] Utafiti wake unahusisha usimamizi endelevu wa mandhari mijini pamoja na usalama wa chakula.[3]
((cite web))
: More than one of |accessdate=
na |access-date=
specified (help)