Dakika ya tao (kwa Kiingereza: arc minute) ni kipimo cha pembe. Inataja sehemu ya 60 ya nyuzi moja.

Dakika 60 za tao zinalingana na nyuzi moja. Nyuzi 360 ni sawa na duara kamili.

Kifupi chake ni arcmin au alama ya '.

Katika upimaji kuna migawanyo midogo zaidi ya dakika ya tao:

Dakika ya tao inalingana na pembe jinsi tunvyoona mita moja kwa umbali wa kilomita 3.44.

Mtazamaji kwenye Dunia anaona mwezi mpevu kwa upana wa dakika za tao 32.

Kizio hiki hutumiwa katika astronomia, upimaji wa ramani na maeneo na kwa kueleza umakini wa kulenga silaha.

Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dakika ya tao kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.