Bud Spencer
Jina la kuzaliwa Carlo Pedersoli
Alizaliwa 31 Oktoba 1929
Kafariki 27 Juni 2016 (miaka 86)
Jina lingine Bud Spencer
Kazi yake wakili, muimbaji, muigizaji

Bud Spencer (jina la kiraia: Carlo Pedersoli; 31 Oktoba 1929 - 27 Juni 2016) alikuwa muigizaji maarufu wa filamu za Kiitalia,

Anafahamika kwa urefu wake wa cm 194 na pia alicheza katika baadhi ya filamu za Spaghetti Westerns. Spencer alikuwa na mafanikio sana kwa kuwa enzi ya ujana wake alikuwa muogeleaji mzuri wa maji, na pia alifaulu digrii ya sheria hata akajisajili na leseni mbalimbali kama mwanasheria.

Wasifu

Bud Spencer alizaliwa kama Carlo Pedersoli mjini Napoli (mtaa wa Santa Lucia). Spencer alimuoa Maria Amato mwaka 1960; kwa pamoja wamezaa watoto watatu: Giuseppe (alizaliwa 1961), Christine (alizaliwa 1962) na Diamante (aliyezaliwa 1972).

Spencer alianzisha kampuni ndogo ya uchukuzi wa mizigo, hasa katika viwanja vya ndege, kampuni ilijulikana kama Mistral Air mnamo 1984, lakini baadae aliachana nayo na kwenda kununua kampuni ya kutengeneza nguo za watoto.

Shughuli za uigizaji

Bud Spencer katika filamu zake za awali alikuwa akiigiza kama moja kati ya walinzi wa falme la Praetoria, katika filamu ya Quo Vadis, ni filamu iliochezwa nchini Italia, mnamo mwaka 1951.

Kwenye miaka ya 1950 hadi miaka ya 1960, Spencer ameonekana katika baadhi ya filamu za kiitalia, lakini bado kazi zake zilikuwa zina ushindani mdogo hadi kufikia mwishoni mwa miaka ya 1960.

Spencer baadae akakutana na mwigizaji filamu mmoja aitwaye Terence Hill, ambaye kwa pamoja wakafanya filamu nyingi tu za Western ya Italia, maarufu kama spaghetti western, na nyingine nyingi, zikiwemo zile walizokuwa wakiziita kwa jina la kimarekani; filamu hizo ni kama zifuatavyo:

  1. God Forgives... I Don't! (1967)
  2. Ace High (1968)
  3. Boot Hill (1969)
  4. They Call Me Trinity (1970)
  5. Blackie the Pirate (1971)
  6. Trinity Is STILL My Name! (1971)
  7. All the Way, Boys! (1972)
  8. Watch Out, We're Mad (1974)
  9. Two Missionaries (1975)
  10. Crime Busters (1976)
  11. Odds and Evens (1978)
  12. I'm For the Hippopotamus (1979)
  13. Who Finds a Friend, Finds a Treasure (1981)
  14. Go For It! (1983)
  15. Double Trouble (1984)
  16. Miami Supercops (1985)
  17. Troublemakers (1994)

Filamu nyingi za aina hii zilikuwa na majina mawilimawili, maana ilikuwa inategemea na nchi yenyewe au msambazaji mwenyewe vile apendavyo. Baadhi zilitolewa katika muundo wa lugha ya Kiitalia na kubadilishwa au kutafsriwa kwa lengo la kwenda kuuza nchi za nje.

Filamu za namna hiyo zilileta mkusanyiko mkubwa wa wagizaji wa filamu kutoka nchi mbalimbali hasa zile za nchi za Ulaya. Kwa mujibu wa IMDB waigizaji hao wa filamu za Kiitalia ambao si wa Italia wametengeneza takribani filamu 19.

Hizo filamu zilizodi (Mbali na zilizorodheshwa hapo juu) Upo uwezekano mkubwa wa kuwa na matoleo mawili ya Kijerumani ya filamu ya "God Forgives... I Don't!" na "Boot Hill" ambayo ilimalizaliwa kabisa, kukata baadhi ya vipande na kuweka jina jipya ili iweze kusukumwa haraka sokoni.

Filamu alimocheza

Bud Spencer na Terence Hill katika moja kati ya filamu za western.

Viungo vya nje