Buabua | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Buabua domo-kubwa
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
|
Buabua ni ndege wa familia Sternidae. Watu wengi huita ndege hawa shakwe kama spishi za familia Laridae. Wengine hutumia jina buabua kwa spishi za jenasi Anous na Chlidonias. Spishi za jenasi Gygis ni nyeupe kabisa, zile za Sterna ni nyeupe na zina utosi weusi; spishi nyingi zina madoa meusi kwa mabawa pia. Spishi za Chlidonias zina zaidi ya rangi nyeusi, hata kwa mwili wao, na spishi za Anous zina rangi nyeupe chache tu. Buabua wana domo refu kadiri lenye ncha kali. Wanaweza kuogelea na wana ngozi kati ya vidole vyao.
Kama shakwe, buabua huhusiswha na pwani, lakini spishi nyingi wanatokea mbali na bahari, kwa kawaida karibu na maji. Huwakamata samaki wakipiga mbizi, lakini spishi za Chlidonias huwakamata wadudu pia kutoka juu ya maji baridi. Hulitengeneza tago lao chini, mara nyingi kisiwani.