Benki ya Ushirika ya Taiwan katika jiji la Taipei

Benki ni taasisi inayoshughulika biashara ya fedha. Shughuli zake za msingi ni pamoja na kukopa na kukopesha fedha.

Kwenye ngazi hii benki inatunza pesa ya watu wengi. Kwa utunzaji huu benki haiachi pesa kukaa bure tu lakini inaitumia kwa biashara yake. Inaitumia kukopesha kampuni au watu wanaohitaji fedha.

Wanaokopa pesa wanalipa riba ambayo ni mapato ya benki kwa huduma ya kukopesha; kutokana na mapato haya benki inalipa pia riba ndogo zaidi kwa wale waliopeleka pesa zao kwake. Tofauti kati ya viwango vya aina hizi mbili za riba ni faida na pato la benki. Jambo muhimu linaloangaliwa na benki wakati wa kukopesha pesa ni uwezo wa mkopaji kurudisha deni lake.

Asili ya benki ilikuwa biashara ya wakopeshaji fedha. Siku hizi kuna benki za aina mbalimbali pamoja na:

Tanbihi

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Benki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.