Bartimayo ni mmojawapo kati ya wachache ambao tunafahamu majina yao kati ya waliofaidika na miujiza ya Yesu, ingawa inawezekana si jina lake mwenyewe, bali ubini kama lilivyotafsiriwa "mwana wa Timayo".[1]
Kipofu huyo alimlilia sana Yesu akimuita "Mwana wa Daudi", bila kujali makemeo ya watu wengine waliomdharau kama mkosefu aliyeadhibiwa na Mungu.
Habari yake inasimuliwa na Injili Ndugu zote tatu mwishoni mwa safari ya Yesu Kristo kwenda Yerusalemu ili kufa msalabani na kufufuka (Mk 10:46-52; Math 20:29-34; Lk 18:35-43).[2][3][4]
Papa Benedikto XVI alifananisha Kanisa lote na Bartimayo, kipofu aliyejaliwa kuona.[5]
![]() |
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bartimayo kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |